Departments

Idara

Idara ya Mitaji ya Umma na Uwekezaji

Idara ya Usimamizi na Usajili wa mali za Umma

Idara ya Rasilimali watu, Utawala na Mipango

Idara ya Mitaji ya Umma na Uwekezaji

Idara hii ina divisheni mbili (2) ambazo ni Divisheni ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma na Divisheni ya Usimamizi wa Mifumo ya Kiutawala na Maslahi.

Majukumu ya Idara

  • Kutayarisha miongozo mbali mbali inayohusiana na usimamizi wa taasisi za uwekezaji na zenye mitaji ya umma.
  • Kuandaa mikataba ya kiutendaji na viongozi wakuu wa taasisi za uwekezaji na taasisi zenye mitaji ya umma.
  • Kushauri juu ya namna bora ya kuongeza mitaji katika mashirika ya umma.
  • Kusimamia uwekezaji wa umma kwa niaba ya Serikali.
  • Kuidhinisha mapendekezo ya uwekezaji wa taasisi za umma.
  • Kufanya uchambuzi wa bajeti za mashirika na taasisi zenye mitaji ya umma.
  • Kuandaa miongozo kuhusiana na utoaji wa gawio na uwasilishaji wa michango katika mfuko mkuu wa Serikali.
  • Kusimamia utendaji wa wenyeviti, wajumbe wa bodi, na watendaji wakuu wa taasisi zinazosimamiwa na Msajili.
  • Kutoa maoni na mapendekezo ya miundo ya taasisi na miundo ya utumishi ya mashirika ya umma na taasisi zenye mitaji ya umma zinazosimamiwa na Msajili kabla ya kuwasilishwa Kamisheni.
  • Kutoa maoni na mapendekezo kuhusu ulipaji wa maslahi na motisha mbali mbali kwa taasisi zenye uwekezaji na zinazosimamiwa na Msajili.
  • Kupitia na kutoa maoni, ushauri, na mapendekezo juu ya miradi mipya/uwekezaji kwa lengo la kukuza mitaji ya umma.
  • Kuandaa na kuingia mikataba ya kiutendaji na viongozi wakuu wa taasisi za uwekezaji na taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili.
  • Kutoa miongozo kuhusiana na bajeti, mipango mkakati na kibiashara, na mambo mengine yanayohusiana nayo katika taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili.
  • Kushauri namna bora za matumizi ya fedha katika taasisi za umma kwa lengo la kupunguza matumizi.
  • Kufuatilia utekelezaji wa taratibu za kuundwa upya kwa taasisi za uwekezaji na zilizo chini ya Msajili.
  • Kufanya ufuatiliaji wa miradi na masuala mbali mbali yanayohusiana na uwekezaji na mitaji ya umma.

Divisheni ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma

Majukumu ya Divisheni

  • Kutayarisha na kuanisha Taasisi za uwekezaji katika madaraja mbali mbali.
  • Kupendekeza mgao wa faida ya mwaka, kutangaza mgao au mchango wa Taasisi za uwekezaji wa Umma.
  • Kuandaa na kusimamia daftari la Taasisi za uwekezaji za umma.
  • Kufanya uchambuzi na tathmini ya miradi mipya inayowasilishwa na Taasisi za uwekezaji wa Umma kwa dhumuni la upatikanaji wa fedha.
  • Kushauri juu ya matumizi ya fedha yasiyokuwa na tija kwa taasisi za uwekezaji.
  • Kufanya na kutoa tathmini za kiutendaji kwa taasisi zenye mitaji ya umma na uwekezaji.
  • Kupokea na kuchambua bajeti, mpango mkakati, mipango ya biashara na kutoa miongozo kwa Taasisi za uwekezaji.
  • Kutoa maoni, ushauri na mapendekezo juu ya kuzisaidia taasisi za uwekezaji wa umma kutoka kwenye vikwazo na hatua sahihi zinazopaswa kuchukuliwa.
  • Kufanya tathmini ya mwenendo wa biashara kwa taasisi za uwekezaji wa umma.
  • Kupitia na kuchambua masuala ya fedha katika taasisi za uwekezaji wa umma na kushauri ipasavyo.
  • Kufanya ukaguzi wa kuangalia mapato na matumizi katika taasisi za uwekezaji wa umma.

Divisheni ya Usimamizi wa Mifumo ya Kiutawala na Maslahi.

Majukumu ya Divisheni

  • Kupitia, kuchambua na kutoa mapendekezo ya miundo ya utumishi kutoka katika taasisi zilizochini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kabla ya kuwasilishwa Kamisheni.
  • Kupitia na kupendekeza masuala ya mishahara na maslahi ya taasisi, wenyeviti, wajumbe wa bodi, watendaji wakuu wa taasisi na watumishi kabla ya kuwasilisha Serikalini.
  • Kufuatilia utendaji wa wenyeviti na watendaji wakuu wa taasisi za uwekezaji na taasisi zisizo za kibiashara zenye mitaji ya umma.
  • Kuandaa mikataba na kuweka vigezo vya kiutendaji kwa wenyeviti na wakuu wa taasisi zilizo chini ya usimamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
  • Kutoa maoni na mapendekezo juu ya kanuni za ndani za taasisi za uendeshaji na usimamizi wa watumishi kabla ya kuanza kutumika.
  • Kupendekeza njia bora na mifumo ya uendelezaji na usimamizi wa utumishi wa mashirika na taasisi zisizo za kibiashara.
  • Kupitia mapendekezo ya muundo wa taasisi kabla ya kuwasilishwa Kamisheni ya Utumishi.
  • Kutoa ushauri na mapendekezo ya uanzishwaji wa taasisi mbali mbali zinazohusiana na uwekezaji na zisizo za uwekezaji.
logo

Anuani za Ofisi

Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

7 Barabara ya Gymkhana Kikwajuni - Mjini Magharibi

info@trosmz.go.tz

+255 24 223 1095

Systems

OTRMIS

GMS

ZGAMIS

Quick Links

Mwanzo

Kusuhu Sisi

Ripoti Mbalimbali

Kituo cha habari

Machapisho

Idara Zetu

Top Sites

Ikulu

Baraza la Wawakilishi

BOT

OR - Fedha na Mipango

Tovuti ya Zanzibar

Msajili wa hazina Tanzania

© 2025 Ofisi ya Msajili Hazina Zanzibar